Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msanii Sofia asimulia alivyong'oa meno kisa tamthilia

Msanii Sofia Asimulia Alivyong'oa Meno Kisa Tamthilia Msanii Sofia asimulia alivyong'oa meno kisa tamthilia

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waswahili husema usione vyaelea ujue vimeundwa, msemo huu una akisi safari ya mwigizaji Afsa Omary maarufu kama Sophia, ambaye ili kuweka uhalisia kwenye Tamthilia ya Jua Kali ya Lamata Leah ilimbidi angoe meno yake mawili ya juu.

Akizungumza na Mwananchi mwigizaji huyo amesema kwa kuwa anapenda kazi yake na ndiyo inamfanya alee familia yake, ilibidi ang'oe meno yake ili kuweka uhalisia na utofauti kwenye tamthilia hiyo kwa kuwa ilihitaji mtu wa aina hiyo.

"Nakumbuka siku ambayo naletewa stori inayohusu kung'oa meno na Lamata nilimwambia mimi naweza kutoa meno, alihoji utawezaje wewe una familia una mchumba siyo rahisi lakini mimi nilimwambia inawezekana.

Siku niliyoamua kufanya hivyo sikumshirikisha mama wala Lamata mwenyewe walishtukia tu siku ya tukio, niling'oa meno mawili ya mbele maumivu yalikuwa makali sana lakini hilo halikunipa shida kwa sababu nilitaka kufanya uhalisia na kazi hii ndio inanipa maisha," anasema msanii huyoa.

Anasema baada ya kutoa meno mama yake na Lamata walishtuka na kutofurahishwa na tukio hilo lakini hawakuwa na chakufanya kwa sababu tayari alikuwa ametoa meno yake na hakuna njia nyingine.

"Mama yangu aliumia sana lakini baadaye akawa upande wangu kutokana na kukubali nilichokifanya kwa lengo la kupata fedha za kuendesha maisha, kwa upande wa mchumba wangu nilimuambia ni maigizo tu sijatoa meno alikuja kutambua baadaye akashtuka sana," anasema Sophia ambaye amekuwa akipambana na Semeni kila mara kwenye maigizo ya ndoa yao. .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live