Baada ya Khaligraph Jones kuamsha tasnia ya mziki wa rap Africa Mashariki ujumla,zimekuepo `diss track' nyingi sana kutoka nchi jirani Tanzania na humu nchini pia.
Wasanii wengi wametoa ngoma nyingi zikimkashifu Jones wengi wakidai amekosea wengi wakimsifu.
Kutoka jijini Nairobi anakotokea msanii GIDI KOCHA pia ni miongoni mwa wasanii waliotoa ngoma kum diss Jones ila hatua hiyo haikupokelewa vizuri na washabiki wake badala yake amekua akipokea jumbe nyingi watu wakimtukana sana, wakukosoa wimbo wake kwamba hakupaswa kufanya hivo.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook GIDI ameamua kuomba radhi Tanzania na Kenya pia kwamba watu hawakumuelewa ila yeye alikua tu na nia njema. Amesema huu ni mziki tuu na kila mtu huvutia kwake kwa lengo la kufikisha mziki mbele.
"Wakenya na Wa Tanzania mnisamehe maana hamkunielewa ila mbona hakuna anayenielewa, hili game tu na kila mtu anavutia kwake amna bifu yoyote bana inakuaje chuki nyingi nyumbani,tupatane basi tuyaweke wazi," amesems GIDI KOCHA.