Mwanamuziki wa Bongo Fleva Bruce amesema wakati yupo #BSS, alikuwa anaumizwa na majibu ya Master J, lakini hadi sasa wapo sawa kwani anaamini alikuwa anamjenga na si vinginevyo.
Bruce anaeleza ubaya ulikuwa Master anavyotoa 'komenti' na inavyomfikia, hasa kuambiwa hamna kitu anasema kama angekuwa legelege angekata tamaa, lakini kwakuwa alijua anachotaka hivyo haikumvunja moyo.
"Ilikuwa inaniumiza sana, hasa kwenye kile kipindi cha ‘All Stars’, ilifika muda nikawa nalia nikifika nyumbani, japo pale mbele nilikuwa nacheka sioneshi ila nikifika nyumbani nalia, yaani muziki nautegemea halafu nakataliwa mbele za watu hadi kuna kipindi nilifikiria kwani nilizaliwa ili nishindanage, ila naamini ilikuwa ni changamoto tu,” anasema #Bruce