Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msami Baby afunguka kumpa mimba Video Vixen

MSAMI.png Msami Baby afunguka kumpa mimba Video Vixen

Mon, 4 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa BongoFleva na mkali wa kucheza Msami Baby amekana madai ya kumpa mimba mwanamke mmoja aitwaye Lizzy ambaye aliwahi kufanya naye kazi wakati wanashoot video yake.

Kupitia show ya Friday Night Live "FNL" ya East Africa TV, Msami Baby amesema mwanamke huyo alikuwa anatafuta engo ya kujulikana kwa sababu sasa hivi yeye hana muda na mapenzi.

"Yule mdada kiukweli namfahamu ila alikuwa anatafuta engo tu kwa sababu yeye ndiyo alifanya ile interview, kulitokea kukosa maelewano kati yetu kwa hiyo ndiyo akaamua kuja na ishu ile lakini sikupita naye" amesema Msami Baby

"Unajua mimi ni mtu wa kuchagua sana wanawake ikija kwenye ishu ya mahusiano siwezi kuwa na yeyote ili mradi tu, na sasa hivi sijaona wa kuwa naye nimeona bora niachane na mapenzi ili nizingatie kutengeneza maisha yangu" ameongeza

Chanzo: www.tanzaniaweb.live