Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msama: Wasanii msinunue magari ya kifahari mkopo wa Serikali

B983DC55 B543 443D A019 1F8EC8679FB3.jpeg Msama: Wasanii msinunue magari ya kifahari mkopo wa Serikali

Sun, 12 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama, amewashauri wasanii kutumia mikopo waliyopewa na serikali kupitia mfuko wa Sanaa na Utamaduni katika kuendeleza kazi zao na kuepuka kuzitumia kununua magari ya kifahari.

Msama ameyasema hayo leo Jumapili Februari 12, 2023 alipokuwa alielezea kurejea kwa tamasha la pasaka ambalo halijafanyika kwa miaka mitano sasa.

Mfuko huo ambao uliwahi kuwepo miaka ya nyuma na kufa kwa sababu mbalimbali ikiwemo wadau kushindwa kurudisha mikopo, ulifufuliwa tena na aliyekuwa Rais wa tano, Hayati John Magufuli, Novemba mwaka 2019 katika kongamano la Sanaa la Mwalimu Nyerere lililofanyika jijini Dar Salaam na tayari baadhi ya wasanii waneshaanza kufaidika baada ya serikali kutengea bajeti ya Sh2.5 bilioni.

Msama alisema serikali imewakumbuka wasanii katika mikopo baada ya kuwepo kwa vikwazo vya kukopesheka kwa muda mrefu kwenye taasisi za fedha, hivyo anaamini fedha hizo wasanii hawatakwenda kushindana kununulia magari na badala yake kufanyia kazi iliyokusudiwa.

"Niwasihi sana wasanii kafanyieni kazi iliyokusudiwa katika mikopo hii,kwani mkichukuwa na kuweza kurudisha kwa wakati ,wengine wengi watakopeshwa na hivyo kuinua sekta yetu ya sanaa nchini," amesema Msama.

Aidha Mkurugenzi huyo amesema ana imani na viongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo akiwemo Waziri Mohamed Mchengerwa na Katibu mkuu wa wizara hiyo, Dk Abbasi kuwa wataisimamia vema na kusababisha sekta hiyo kuzidi kukuwa na kizidi kuaminiwa na watu na taasisi mbalimbali.

Kuhusu tamasha la Pasaka Msama amesema linarudi ikiwa ni miaka mitano imepita tangu halijafanyika. Amesema tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Aprili 9 mwaka huu ambapo eneo litakapofanyika na wasanii wa kitaifa na wa kimataifa watakaohidhuria wataanza kutangazwa kuanzia wiki ijayo.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati maandalizi ya tamasha hilo, Emmanuel Mwabisa amesema wamejipanga vizuri na tayari wameshaanza kufanya mazungumzo na wasanii wa nchi mbalimbali ikiwemo Rwanda, Congo, Kenya, Uganda, Uingereza na Afrika Kusini.

Chanzo: Mwanaspoti