Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrisho Mpoto awaliza Watanzania, Amuomba Kingunge afikishe salamu hizi kwa Mwl. Nyerere (+video)

Wed, 7 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa nyimbo za asili na mtaalamu wa kughani nchini Tanzania, Mrisho Mpoto ameomboleza kifo cha Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru kwa kumuomba afikishe salamu za Watanzania kwa Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere kuwa rushwa bado inalitafuna taifa letu.

Mrisho Mpoto

Mpoto akiwa mwenye uso wa huzuni katika viwanja Karimjee leo Jumatatu Februari 5, 2018 jijini Dar es salaam akiuaga mwili wa Kingunge, amesema kuwa Kingune akienda huko mbinguni akakae na Mwl. Nyerere wajadili tathmini yao juu ya rushwa kwani ingawaje waliweka nguvu kubwa kutokomeza lakini wimbo huo bado unaimbwa nchini.

Tazama video hapa chini akighani kwa ustadi mashairi yake mbele ya Watanzania.

Chanzo: bongo5.com