Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrisho Mpoto atoa msaada kwa yatima, awapa msingi wa maisha (Video)

1892 Screen Shot 2018 01 24 At 19.03.49.png

Thu, 25 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto kwa kushirikiana na team yake ya Mpoto Foundation alitembelea kituo cha watoto yatima cha Mwandaliwa na madrasa ya Tidaiya iliyopoTandale.



Akizungumza na waandishi wa habari wakati akikabidhi zawadi hizo, Mpoto alisema lengo kubwa la kutoa zawadi hizo ni kusaidia malezi ya watoto katika vituo hivyo ili wakue wakiwa katika maadili mazuri.



Mkurugenzi wa Kituo cha Mwandaliwa, Halima Ramadhani (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na zawadi alizozipokea kutoka kwa Mpoto.

“Nimeamua kugawana na watoto kidogo nilichojaliwa nacho ili waweze kufurahi lakini pia kuwasaidia katika makuzi hasa kwenye suala zima la kidini na maadili.” alisema Mpoto.

Aidha Mpoto aliongeza kuwa kutokana na mambo mengi yanayoendelea kwa sasa nchini na duniani kote, kuna uwezekano kwa watoto kukua bila misingi mizuri ya dini, heshima na uzalendo kama wasipoandaliwa mazingira mazuri.

Ili kuhakikisha hilo halitokei, Mpoto amesema imekuwa sababu kubwa iliyompelekea kujitolea zawadi hizo ambapo kwa yeye ni kuufungua mwaka 2018 akiwa na thawabu kutoka kwa watoto.



Mpoto akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa madrasa ya Tidaiya iliyopo Tandale.

Chanzo: bongo5.com