Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrembo kutoka Kenya afunguka A-Z ishu ya kupewa ujauzito na Harmonize

7839 Zqw BONGO5 PIX TZW

Fri, 11 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Mrembo kutoka nchini Kenya ambaye pia ni msanii wa muziki wa Injili, Veronica Wanja ‘Nicah The Queen’ amefunguka ukweli wa taarifa zilizodai kuwa amepewa ujauzito na msanii Harmonize kutokea WCB.



Muimbaji huyo ametumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuwaomba radhi mashabiki wake kufuatia kuenea kwa taarifa hizo na kueleza kuwa yeye si mjamzito na picha yake iliyosambaa akiwa na Harmonize walipiga mwaka jana studio na tangu hapo hawakuonana tena.

‘I owe all my fans the truth and an apology for all those who support my ministry, I have never been into a relationship with Harmonize, I’m not pregnat . We took this photo sometime last year at the studio, I have never met him again ever since.” amesema Nicah The Queen.

Ameendelea kwa kusema kuwa anafahamu kuwa Harmonize yupo katika mahusiano na msichana wake na amekuwa akiupenda muziki wake kwani ni msanii ambaye anajituma sana ila hakuna chochote kati yao.

“Harmonize is in a loving and serious relationship with his girlfriend. I admire his hard work and I like his music. There’s nothing between me and him,” amesisitiza.

Kwa kipindi kirefu sasa Harmonize amekuwa katika mahusiano na mpenzi wake Sarah, hajawahi kukumbwa na skendo ya kutoka na mwanamke mwingine zaidi kutupiana maneno ya hapa na pale na ex-girlfriend wake, Jacqueline Wolper.

Loading...
Chanzo: bongo5.com