Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrembo azimia baada ya kudukua simu ya mpenzi wake

Fb Haki Mrembo azimia baada ya kudukua simu ya mpenzi wake

Thu, 22 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo mmoja aliyefahamika kwa jina la Bongiwe Indlovukazi huko Afrika ya Kusini amejikuta katika wakati mgumu baada ya kudukua simu ya mpenzi wake.

Unaambiwa hali hiyo imesababishia Bongiwe maumivu makali kupoteza fahamu mara kadhaa kila siku kutokana na alichokutana nacho kwenye simu.

Bongiwe kupitia ukurasa wake wa Twitter ameeleza hali hiyo aliyokutana nayo ya kuzimia na kuamka ingawa bado hajasema haswa kipi amekutana na nacho kwenye simu ila amekazia tu kwamba wanaume wasikie tu.

"Nilidukua simu ya mpenzi wangu, nimekuwa nikizimia na kuamka siku nzima," aliandika Bongiwe huku akiweka video na kumwaga machozi wakati akielezea tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live