Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mrembo aliedai kaokoka ili achumbiwe kamaliza kreti bia

POMBE 640x400 Mrembo aliedai kaokoka ili achumbiwe kamaliza kreti bia

Sat, 3 Oct 2020 Chanzo: millardayo.com

Jamaa mmoja nchini Kenya ameachwa mdomo wazi baada ya mwanamke aliyedhani ameokoka kunywa kreti nzima ya pombe chini ya saa mbili baa zilipofunguliwa.

Inasemekana kwamba jamaa huyo na mwanamke huyo ambaye ni mpenzi wake waliingia baa kula na baada ya kumaliza mlo mrembo aliomba aletewe chupa moja ya bia.

Hata hivyo jamaa hakukubaliana na ombi la mrembo huyo “Beib unajua vizuri mimi sipendi kulewa tena uliniambia kuwa wewe si mlevi umeokoka, inakuaje leo unataka pombe?” jamaa alimuuliza mrembo.

Mwanamke huyo alimfungulia roho jamaa na kumfichulia kwamba awali alikuwa akinywa kisha akaacha “Tulipoanza kuchumbiana niliacha kunywa pombe, lakini sijui kiu imetoka wapi, ninataka kuonja tu kidogo,”. 

Jamaa akaagiza bia chupa moja “Baby chupa moja haitoshi, naomba kuongeza nyingine kwa bill yangu,” mwanamke huyo alimuomba mpenzi wake.

Jamaa alimuagizia chupa zingine mbili ambazo mwanamke huyo aliziporomosha kama maji bila hata kujali “Kwani wewe hii pombe unakunywa aje kama maji,” jamaa alimuuliza mrembo.

Hata hivyo, mrembo huyo hakujali jamaa alicheka na kumuita mhudumu “Hii pombe yenu ni tamu sana, leta kreti uiweke hapa, itakuwa rahisi kwangu kutoa hapa chupa moja moja pole pole badala ya kukuita kila wakati,” mrembo alimueleza mhudumu wa baa.

“Wewe beib, unamaamisha utamaliza pombe hiyo yote?! Mimi sasa nataka kuondoka,” jamaa alimkaripia mrembo huyo.

Taarifa zinasema kwamba mrembo huyo alimpuuza barobaro akapanga chupa zote za pombe kwenye meza na kuanza kunywa moja baada ya nyingine hadi kreti nzima ikaisha.

Inasemekana jamaa aliachwa ameduwaa na kuamka pole pole akashika njia na kuondoka “Itisha kreti nyingine kama unataka sasa,” jamaa alisema akiondoka.

RAIS MAGUFULI ALIVYOTUA ZANZIBAR

Chanzo: millardayo.com