Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrembo alichoma moto wigi alilozawadiwa na mpenzi wake

Wigi As Mrembo alichoma moto wigi alilozawadiwa na mpenzi wake

Fri, 16 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo mmoja amewaacha watumiaji wa mitandao ya kijamii katika butwaa la karne baada ya video yake kuonekana akilichoma wigi alilonunuliwa kama zawadi na mpenzi wake kwa madai kwamba ni la bei rahisi ikilinganishwa na hadhi yake.

Katika video iliyopostiwa kwenye Instagram, mrembo huyo aliyefahamika kwa jina la Elizabeth raia wa Nigeria inaarifiwa ndiye aliposti video hiyo akilichoma wigi hilo.

Baada ya kuliteketeza kwa moto, mwanadada huyo alibeba mabaki na kutupa kwenye rundo la takataka nje ya nyumba yake.

Mwanamke mwingine ambaye alifikiri kuwa mwanamke huyo alikuwa amemkasirikia aliyemuuzia wigi alimhimiza amfichue muuzaji huyo wa nywele ili wengine wamuepuke.

Lakini alieleza kuwa muuzaji hakufanya kosa lolote, bali ni mpenzi wake ndiye aliyempatia wigi kwa sababu hajui lile la ubora.

Kitendo hicho kiliwafanya baadhi ya wanamitandao kuona mwanamke huyo kama mtu asiye na shukrani ya kuridhika na kile kidogo alichopewa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live