Menu ›
Burudani
Thu, 26 Sep 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Watu wawili wamekamatwa nchini Uingereza kufuatia kifo cha mwanamke anayesadikiwa kufanyiwa urekebishaji wa kuongeza makalio usiohusisha upasuaji.
Alice Webb, 33, alifariki katika Hospitali ya Gloucestershire asubuhi ya Jumanne, baada ya kuanza kujihisi vibaya.
Watu hao wawili waliotuhumiwa kuua bila kukusudia, wameachiliwa kwa dhamana ya polisi huku uchunguzi ukiendelea kufanyika.
Tukio hili litakuwa la kwanza kutokea nchini Uingereza kwa urekebishaji umbo kwa njia isiyo ya upasuaji.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live