Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrembo afa kwa moto baada ya kuteketeza nyumba akigombana na mumewe

Bimbo IVD Mke afa kwa moto akigombana na mumewe

Thu, 20 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wasahili wanasema hasira hasara! Bimbo; ni mama wa watoto sita na mke wa mfanyabishara maarufu nchini Nigeria aitwaye Ikechukwu Ogbonna almaarufu IVD ambaye amekuwa kwenye ndoa kwa miaka 22 kabla ya kufariki dunia baada ya kuungua vibaya.

Kwa mujibu wa mtandao wa Lindaikeji, Bimbo alikuwa anakabiliwa na unyanyasaji uliokithiri kutoka kwa mumewe huyo ambaye huwauzia mastaa wengi magari nchini humo.

Wikiendi iliyopita, Bimbo alidaiwa kumgombeza mumewe akimuuliza kwa nini amekuwa akimpiga kwa miaka mingi na kumyanyasa ambapo ugomvi uliibuka tena na kusababisha nyumba yao kushika moto.

Bimbo alidaiwa kuchoma nyumba na aliungua vibaya mno na kukimbizwa hospitalini ila mumewe alipata majeraha kidogo tu.

Mwanamke huyo alifariki dunia Ijumaa ambapo dada yake, akiwa akiwa analia ameibuka na kumshutumu shemeji yake huyo kuwa ndiye chanzo cha kifo cha Bimbo kwa kumsukuma kwenye moto halafu akawa anamchukua video akiungua.

Baada ya mkewe kufariki dunia, mume huyo aliposti videos kadhaa mtandaoni huku akiwa hajali mkewe kufariki dunia ila alikuwa anaonesha kusikitishwa nyumba yake kuungua na kupata hasara.

Pia amelalamikia mkewe kuharibu gari na katika moja ya video, sauti ya mke inasikika akieleza kuwa mume wake huyo tayari ni muathirika wa Virusi Vya Ukimwi (VVU) na anajihusisha na nguvu za giza ili apate utajiri.

Kwa miaka kadhaa, Bimbo amekuwa akieleza kupitia unyanyasaji na kupigwa mno ndani ya ndoa yake ambapo mwaka 2019 alielezwa kupigwa na mumewe huyo hadi kuwa katika usingizi wa kifo (coma) huku akiwa mjamzito wa miezi 8, lakini bahati fahamu zake zilimjia baadaye.

Mwaka 2020 aliibuka tena na kueleza kupigwa tena na kusema amenyanyaswa mno kwa miaka 19.

Januari mwaka huu 2022, Bimbo aliibuka tena mtandaoni na kusema kwamba afya yake ya akili haipo sawa na kuwataka watu wamsaidie kuwachukua watoto wake 5 huku akimlaumu mumewe huyo kuyaharibu maisha yake hivyo kuhofia na watoto wake kutokuwa salama.

Alisema kuwa, kuna wakati mumewe alikuwa anamnyooshea bastola mbele ya watoto wao. Pamoja na kueleza kila wakati kuwa ananyanyasika na kusalitiwa, lakini aliendelea kubaki ndani ya ndoa hadi mauti yamemkuta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live