Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Mrembo adaiwa kumuua mpenzi wake wakati wakifanya mapenzi

DEATHSEX Mrembo adaiwa kumuua mpenzi wake wakati wakifanya mapenzi

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winfred Mueni (28) amefikishwa katika Mahakama ya Makadara jijini Nairobi, akishtakiwa kwa mauaji ya kutokusudia baada ya mpenzi wake Titus Njoroge Kimani (30), kufariki dunia wakati wa tendo la ndoa.

Tukio hilo linadaiwa kutokea nyumbani kwa marehemu katika Mtaa wa Baba Dogo, Ruaraka, jijini humo.

Mtandao wa Taifa leo umeripoti kuwa Mueni anashtakiwa kwa kufupisha maisha ya mpenzi wake Septemba 22, 2023, ambapo inadaiwa kuwa wakiwa katika tendo ndoa, na hasa wakati Kimani anafika kileleni, alipoteza fahamu na kuanguka.

Inadaiwa kuwa kuwa Winfred alijaribu kuokoa maisha ya mpenzi wake kwa kumpeleka hospitali, hata hivyo, baada ya kufika, alielezwa kuwa Kimani amekwishafariki.

Kwa mantiki hiyo, mahakama hiyo imeelezwa kuwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP), inamshtaki Winfred, kwa kile kinachodaiwa kuwa ni “mtu wa mwisho kuonekana na marehemu” kabla ya kifo chake.

Sheria ya shtaka hilo, inatoka hukumu ya kesi katika Mahakama Kuu ya Nigeria, ambapo Mkuu wa Sheria nchini humo, alimstaki Stephen Haruna kwa mauaji ya aliyekuwa bosi wake mwaka 2012.

Uamuzi huo wa mahakama hiyo, ulimfuka Haruna Oktoba 6, 2008 kwa kosa la kusababisha maafa.

Kwenye kesi hiyo, Haruna ambaye alikuwa mlinzi katika makazi ya marehemu, alikutwa na hatia ya mauaji kwa msingi wa kuwa ni yeye pekee aliyekuwa kwenye makazi hayo wakati wa kifo cha bosi wake kinatokea.

Mahakama ilibaini kwamba hakukuwa na ushahidi wa kuvunjwa kwa mlango wa makazi hayo na kwamba Haruna alikuwa ndiye mtu pekee kwenye makazi hayo.

Hivyo basi, katika kesi ya Nairobi, ODPP wanaamini kwamba Winfred anastahili kushtakiwa kwa msingi huo, akisema kesi yake inafanana na ya Haruna, licha ya kuwa hakuna ushahidi wowote kuonyesha kwamba alimsababishia mpenzi wake majeraha wakati walipokuwa wanafanya mapenzi.

Upande wa mashtaka umeorodhesha mpira wa kondomu uliotumika ambao ulipatikana kando ya kitanda na ripoti ya kitabibu kama ushahidi mkuu dhidi ya Winfred na mpenzi wake imeorodheshwa kama ushahidi dhidi yake.

Inadaiwa kuwa kisa hiki ambacho kimekuwa kikichunguzwa kwa zaidi ya mwezi mzima kimeleta mgongano baina ya maofisa wa upelelezi kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na wale wa ODPP.

Baada ya uchunguzi wa kina, DCI walikuwa wamependekeza vikao vya wazi vya kubaini alivyofariki Kimani kwa sababu hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja ambao ungemhusisha mtu yeyote.

Kwa mfano, mwili wa Kimani haukuwa na majeraha yoyote wakati ambapo marafiki, nduguy na jamaa zake walifika na kuuta kitandani muda mfupi baada ya Winfred kuwajulisha tukio hilo saa mbili asubuhi.

Maofisa wa upelelezi wa DCI ambao walifika nyumbani ya Kimani mara baada ya kujulishwa na uongozi wa hospitali kwamba Kimani ameshafariki, walikuta kila kitu kikiwa mahali pake.

Nyumba yake ilikuwa na kitanda, viti na mahali pa jikoni na hakukuwa na dalili zozote za mvurugano.

Lakini ODPP waliwakosoa wenzao wa DCI kwa kutochukua chembechembe za mwili wa mwendazake zikakaguliwe kubaini haswa kilichomuua na ndipo akapendekeza Winfred ashtakiwe kwa mauaji ya kutokusudia.

Maafisa wa upelelezi wanaofahamu kuhusu kisa hiki na ambao hawakutaka majina yao yatajwa kwa kuwa siyo wasemaji, wamesema kwamba hakukuwa na haja ya kuchukua chembechembe kwa sababu ripoti ya kitabibu tayari ilikuwa ishabaini chanzo cha kifo cha Kimani.

Kwa upande mwingine Dk Peter Ndegwa, mwanapatholojia aliyefanya uchuguzi wa mwili wa marehemu, katika mochwari ya Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya KUTRRH alibaini kwamba Kimani alifariki kutokana na jeraha la kichwani lililosababishwa na kifaa butu.

Inadaiwa kuwa siku ya tukio Winfred alikwenda nyumbani kwa Kimani, ambapo alikutana na kaka mkubwa wa Kimani pamoja na mjomba wake ambao aliwasalimia na kuzungumza kwa kifupi kabla ya kuingia ndani.

Inadaiwa baada ya Winfred kufika, Kimani aliondoka kwenda kununua pakiti ya kondomu na akarejea kisha wakaanza kurushana roho.

Lakini kwa bahati mbaya, kulingana na maelezo ya Winfredi kwa DCI, inadaiwa kuwa wakati Kimani alipokuwa anafika kileleni, alianza kupatwa na matatizo ya kupumua, akaanza kukohoa na kuishiwa na nguvu akiwa amemlalia.

Aliambia wapelelezi kwamba aliendelea kuishiwa na nguvu hata zaidi na akazimia na kugonga kichwa kwenye fremu ya kitanda na kupoteza fahamu.

Baada ya kuona hivyo, Winfred alitoka mbio huku akipiga mayowe na kuita ndugu wa mpenzi wake ambao walimpata akiwa hana fahamu na akiwa uchi.

Alikimbizwa hospitalini ambapo alipatikana kwamba ashafariki na jamaa wakamsindikiza Winfred katika kituo cha polisi cha Ruaraka ambapo aliwekwa mahabusu.

Alifikishwa katika Mahakama ya Makadara Novemba 10 ambapo alikanusha mashtaka mbele ya Hakimu Mkuu Hellen Okwani. Akaachiliwa kwa dhamana ya KSh500, 000 (takriban Sh8.2 milioni).

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Februari 22, mwakani ambapo itatajwa, huku ikipangwa kusikilizwa kuanzia Mei 30, 2024.

Ndugu wa marehemu Kimani ambao walimuona Winfred akiingia nyumbani kwa humo, lakini pia wafanyakazi wenzake ambao walifika nyumbani alipopiga mayowe wameorodheshwa kuwa mashahidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live