Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrembo acharuka kuzaa mtoto asiyefanana nae

Stephny Ike Mrembo acharuka kuzaa mtoto asiyefanana nae

Thu, 29 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke aitwaye Stephny Ike ameshangaza wengi baada ya kulalama vikali kuhusu mtoto wake kutomfanana.

Mwanamke huyo, kupitia video aliyoposti kwenye ukurasa wake wa Tiktok, anasema kuwa, mtoto wake hafanani naye kama alivyokuwa akitarajia, badala yake amefanana mno na baba’ke.

Stephny analalamika kwamba hiyo ilikuwa kama hujuma kutoka kwa mtoto wake baada ya kumbeba kwa zaidi ya wiki 40 na siku kadhaa.

Mama huyo mpya anasema kuwa, mtoto wake huyo ambaye alimbeba miezi tisa tumboni mwake, ametoka akiwa amefanana zaidi na mumewe kuliko yeye.

Katika video hiyo, Stephny anasema kuwa, anapaswa kulipwa na baba wa mtoto huyo kwa uharibifu wa kihisia ambao ameupitia.

Wengi baada ya kuona video hiyo wamesema kuwa, watoto kufanana na mama au baba kuna faida zake na wengine wakisema haijalishi.

“Nilikubeba kwa miezi tisa ndiyo uje kutokea kufanana kabisa na baba’ko? Alinifanyia ubadhirifu baada kumbeba kwa wiki 40 na siku tano juu,” Stephny ameandika chini ya video hiyo na kuongeza; “Hii siyo haki, wanahitaji kunilipa kwa uharibifu wa kihisia.”

Katika picha ya pamoja ya baba na mtoto huyo, kwa kutazama mara moja tu, unaweza ukakubaliana naye kwamba ni moja kwa moja mtoto ana mfanano wa baba mtu.

Wengine wanasema kwamba kama ni mtoto wa kike ni sawa kwani inatarajiwa hivyo kuwa watoto wa kike aghalabu huchukua sura na tabia za baba huku wa kiume wakichukua sura za mama zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live