Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mr Nice mkali asiyechosha kumsikiliza (Sehemu ya Pili)

MR Nice: Hakuna Anayeweza Kunizidi Rekodi Za Mauzo.png Mr Nice mkali asiyechosha kumsikiliza (Sehemu ya Pili)

Wed, 27 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SEHEMU YA PILI,

Tukirudi katika nyimbo za Mr Nice, Utaona ni kwa namna gani zilimsaidia kujenga urafiki wa kudumu na watoto kuanzia wakiwa wadogo. Na ndiyo maana Jina lake limeendelea kuwepo mpaka leo hii, kuna mengi sana ya kumuelezea Mr Nice, Ni mwamba fulani ambaye alikuwa akipiga Muziki wa kuburudisha zaidi, Na hichi ndicho kilichompa heshima, na kujikuta akipata mialiko mingi.

Ya ndani na nje ya Nchi, Waliomualika walikuwa wanajua kwamba, tukimleta Mr.Nice hapa tutapata show nzuri na ya heshima isiyo ya kihuni. Huwezi kumfukuza mtoto kwa sababu wimbo wa Mr.Nice umeanza kupigwa.

Mr Nice ndiyo Msanii ambaye alikuwa akilipwa ghali zaidi ni msanii aliyelipwa ghali zaidi kwa kila tamasha,kuliko msanii yeyote Afrika Mashariki. Ukweli ndiyo huo. Alikuwa analipwa dola 7000 kwa show za nje ya nchi. Kwa Tanzania ni dola 1500.

Promoters wa muziki nchini walikuwa wanafahamu kwamba ukimleta Mr.Nice atafanya show nzuri,watu watafurahi na hela yake itarudi.

Mr Nice ni msanii mwenye historia ya pekee Afrika Mashariki na kati, Sehemu kama Comoro Burundi na Botswana, Mr Nice alikuwa akipokelewa kama Mfalme, pindi afikapo huko kwa ajili ya Shoo au Mambo yake binafsi, na siyo huko tu bali hata Kenya Uganda na Rwanda, Mambo yalikuwa ni hivyo hivyo, mwamba alikubalika sana katika Nchi hizo, na hata katika Nchi yake ya Tanzania, Katika wimbo wa Kikulacho" Mr Nice alitufundisha namna ya kumuepuka rafiki mnafki, pale aliposema,

Sintojali mimi bado nasonga mbele Ni Mshamba huyo, muacheni apige kelele, Najua kelele za Chura, hazimnyimi tembo kunywa maji, Na dua la kuku halimpati mwewe, Utalijua jiji lololo aah,

Mr Nice anasema kelele za Chura hazimnyimi tembo kunywa maji, Akiwa na maana mtu hata aongee vipi hawezi kukuzuia kufanya mambo yako, Anaposema dua la kuku halimpati mwewe, Anamaanisha kwamba alilolipanga Mungu binadamu hawezi kulizuia, Katika wimbo wa Rafiki" hapa Mr Nice anamkumbusha Rafiki yake, kuhusu yale waliyofanya wakati akiwa na pesa, pale aliposema kwenye Verse ya kwanza,

Ninapokuwa mimi na pesa Tunakula, kunywa na kusaza, Mungu wangu nijalie adui awe rafiki yangu, Maisha safari ndefu yataka moyo wa uvumilivu, Kupata na kukosa, aliyeumba ni muumba, Naomba nisamehe, kama nimekukosea, Nami nitakusamehe kwakuwa ni rafiki yangu,

Hapo Mr Nice alitaka rafiki yake atambue, Kuna wakati mifuko itachacha hivyo isiwe sababu ya kumkasilikia, Akumbuke kuwa kuna wakati alikuwa na pesa na walikula kunywa na kusaza, Katika maisha kuna kukoseana, hivyo Mr Nice amemkumbusha rafiki yake, kama itatokea kamkosea amsamehe na yeye pia atamsamehe maana ni rafiki yake, kuna mengi sana ya kuyachambua kwenye nyimbo za Mr Nice, sidhani kama naweza kutumia siku moja kuweza kukamilisha kazi hiyo, ya kuzichambua nyimbo za Mr Nice, au hata kuelezea Historia yake kwa ujumla, labda niwe mkweli tu kwa wasomaji, Niwaambie tu kuwa, mimi hapa nasimulia kwa uchache Historia ya Mr Nice, Maana Historia ya Mr Nice ni kitabu kizima, na siwezi kuandaa kitabu cha Mr Nice pasi na kumshirikisha yeye ambaye ndiye muhusika,

Upande wa pili, namaanisha nje ya Muziki, Mr Nice alikuwa na mambo mengi sana, mazuri na mabaya, Haya nitakuja kuyaelezea katika toleo linalofata ambalo ni la Mwisho, Nitaeleza namna Mr Nice alivyoingia katika bifu na Dudu baya, Na ilitokea nini mpaka kufikia hatua ya kupigwa na Dudu baya, akiwa juu ya Steji,

Itaendelea

Chanzo: www.tanzaniaweb.live