Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mr Nice mkali asiyechosha kumsikiliza (Sehemu ya Kwanza)

MR Nice: Hakuna Anayeweza Kunizidi Rekodi Za Mauzo.png Mr Nice mkali asiyechosha kumsikiliza

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika kizazi cha hivi karibuni. Wameibuka wasanii wengi sana. Lakini jina la Mr Nice litabaki kuwa juu, kutokana na yale ambayo ameyafanya enzi hizo akiwa katika ubora wake.

Mr Nice nimzaliwa wa Rombo mkoani Kilimanjaro. Aliyaanza masomo ya Shule ya msingi Ilala Boma jijini Dar-es-salaam, kabla hajaelekea tena Moshi kusoma katika seminari ya Maua.

Mr Nice hakuiba Kipaji cha Muziki. Bali alizaliwa nacho, Muziki ulikuwepo kwenye damu yake, hata harakati za kuingia kwenye ulingo wa Bongo Fleva, zilianzia kanisani, Mr Nice alikuwa ni mwimbaji mzuri sana wa kwaya makanisani, kuanzia zile za watoto.

Unataka kujua ni Kanisa gani ambalo Mr Nice alihudumu kwenye kwaya? Ni pale kanisa la Msimbazi Automatically.

Mwaka 2000 ndiyo mwaka ambao Mr Nice alianza rasmi kuimba nyimbo za kidunia, Mwanzoni alikuwa hajiamini sana, na haukuuchukulia Muziki kama career yake. Alikuwa anaimba kama hobby.

"Friday Night" huo ndiyo wimbo wa Kwanza wa Mr Nice, na ndiyo uliompa mwongozo na msukumo wa kuweza kufanya kazi za muziki, maana ulipendwa ghafla bila hata yeye mwenyewe kujua.Kipindi hicho alikuwa anaishi na mama yake mzazi visiwani Zanzibar.

Wimbo wa Friday Night" aliurecodia Dar Es Salaam Mawingu Studio kwa Bony Luv, Bony Luv ambaye ni mmoja wapo wa maproducer wa mwanzo kabisa hapa Tanzania, yeye na Mr Nice walikuwa ni marafiki wa siku nyingi sana.

Turudi katika wimbo wa Friday Night" Mr Nice baada ya kuurecodi aliuacha Studio, na yeye kurudi zake Zanzibar.

Huku nyuma Bony Luv ambaye aliukubali sana ule wimbo wa Mshikaji wake, Akaupeleka redioni bila hata ya kumshirikisha Mr Nice, Kilichotokea ni kwamba wimbo ukaanza kupendwa bila hata kumjua mwimbaji wake ni nani.

Wakati huo Mr Nice yupo zake Zanzibar, naye hajui kinachoendelea, ghafla akaanza kuitwa kwenye interviews mbalimbali na matamasha nk. Huo ndio ukawa mwanzo wa Mr Nice kujiingiza rasmi katika muziki.

Lakini akiwa tayari ameshausoma mchezo na kujua unaenda vipi, Wakati huo wasanii wengi wa Tanzania walikuwa wanarap na kufanya style za hip hop.

Sasa alichokifanya Mr Nice nyimbo zake akawa anaimba haikuwa R&B, bali alikuwa akifuatisha uasili, na ndiyo maana ukitazama nyimbo zake utakuta kuna mambo ya uasili, hususani katika beats ambazo zipo kwenye uasili zaidi na sio commercial kama walivyokuwa wanafanya wasanii wengi wa hip hop.

Na ndipo akaamua kuuita TAKEU, ambapo TA inasimama badala ya Tanzania na KE kwa Kenya na U kwa Uganda.

Hapo utaona kuwa Mr Nice alikusanya tamaduni za nchi hizi tatu, za Afrika Mashariki na kuziweka pamoja. Na utaweza kuona kwamba baada ya hapo wasanii wengi pia walikuja kuhamasika na kuanza kuimba wakitumia style hiyo.

Mr Nice aliona kuimba TAKEU itamfanya kueleweka kwa haraka sana kwa Afrika, tofauti na styles zingine kama hip hop ambazo kila mtu alikuwa anajua kwamba ni ya kimarekani.

TAKEU ilimsaidia sana Mr Nice katika kujimarket na ndiyo maana utaona ilikuwa ni rahisi kwake kupata show za nje. Hiyo ilitokana na uimbaji wake na hata uchezaji wake pia.

Unaweza kujiuliza inakuwaje Mr Nice aishike Afrika mashariki na kati, kwa tungo anazotumia katika nyimbo zake, ambazo ni maneno ambayo yamezoeleka kwa watanzania tangu enzi na enzi, Nyimbo kama Kidali Po, Kikulacho nk?

Maneno ambayo yalitumika hapo ni Maneno ambayo tulishayazoea enzi hizo, hata kabla hatukumjua Mr Nice. Jibu ni kwamba Mr Nice alijua kucheza na akili zetu sisi mashabiki.

Kivipi? Kwasababu Mshikaji alijua anapendwa sana na watoto wadogo. Na hata watu wazima wenye heshima zao pia walikuwa wakimpenda.Kwahiyo hapo ilikuwa ni lazima ajitahidi kukidhi haja ya makundi hayo mawili ya watu kwa wakati mmoja.

Kwahiyo alipokaa chini kutunga Mashairi yake, alihakikisha kwamba kama baba mama na mtoto wamekaa sebuleni, wanaweza kuwa huru kusikiliza nyimbo zake, au hata kumuangalia kwenye video, Hakutaka kuweka yale maneno mazito, maneno ambayo mzazi hawezi kukubali mtoto wake akasilikiza au mtoto hawezi kuyasikiliza mbele ya wazazi wake au akaangalia mbele ya wazazi.

Wasanii wengi wa sasa nyimbo zao, maneno yanayosikika yamewatenga watu katika makundi fulani fulani. Lakini Mr Nice alikuwa yupo kote kote. Mfano ukichukulia nyimbo kama kidali po, kila mtu aliimba, babu bibi na wazazi wetu waliimba, ni wimbo ambao hata usipoupenda wewe mwanao anaweza akakushawishi ukaupenda.

Maana Ukiusikiliza ulikuwa unakumbusha jambo fulani au enzi fulani. Alichojaribu Mr Nice ni kuepuka kurekodi wimbo ambao watu watashindwa kuangalia au kusikiliza mbele za watu kwa sababu ya kuona aibu, jambo ambalo lingemfanya mtu asiwe na jinsi zaidi ya kuzima TV au redio.

Itaendelea.....

Chanzo: www.tanzaniaweb.live