Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mr. Nice awachana Wabongo, awapa tano Wakenya

MR Nice: Hakuna Anayeweza Kunizidi Rekodi Za Mauzo.png Mr. Nice

Tue, 2 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Lukas Mkenda maarufu kama Mr. Nice amewabomoa Watanzania kwa kumzushia mambo mengi huku akiwapa shavu Wakenya kwa ukarimu wako.

Staa huyo mwanzilishi wa TAKEU Style amesema; “Nahisi ningebaki Bongo, ningeweza kufa kwa stress maana mtu anajifanya amesahau hata nyimbo zako wakati nchi ya jirani wanazipenda na hata kukupa shoo.

"Wabongo wengi kazi yao kubwa ni uzushi tu na si kitu kingine chochote,” Mr Nice amesema.

Mr Nice anasema kwa sasa amepata mafanikio makubwa kiasi cha kuweza kuanzisha mradi wake wa maji ya kunywa ambayo yanaitwa Nice Water.

“Haya mafanikio nimeyapata kutokana na kazi yangu ya muziki, siyo kitu kingine chochote.

“Ndiyo maana natamani sana kuendelea kuishi hapa Kenya kwa sababu ndipo ninapopata heshima na kazi yangu ya muziki niliyoifanya kwa zaidi ya miaka 20 naona inaniweka pazuri,” alisema Mr. Nice.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live