Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mr. Nice alitaka nimpe elfu 20 kwa ajili ya wimbo - DJ JD

Mr. Nice DJ JD DJ John Dillinga.

Fri, 12 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JD mkongwe wa Bongo, DJ John Dillinga amesema kuwa, mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Mr. Nice alimuomba pesa kiasi cha Tsh 20,000 kwa ajili ya kununua wimbo wake.

DJ DJ amesema hayo wakati akihojiwa kwenye kipindi maalum cha Salama Na kuhusu masuala mbalimbali ya muziki huo.

"Nyimbo ya kwanza ya Mr. Nice niliikuta imetupwa nikaisikiliza nikaona mbona kama iko sawa hii, Nikaichukua nikaanza kuipiga Redioni. Lakini baadae ilivyokuwa inaendelea kufanya vizuri nilifanya first non-stop Bongofleva, kwa hiyo ikabidi niwa-contact baadhi ya wasanii ili kuweza kuweka mule.

"Sasa Mr. Nice mwenyewe nilipomtumia taarifa aje alikuja alipokuja nikamwambia nataka kununua wimbo wako akasema hapana kaka hamna shida unaweza ukaichukua nikamwambia hapana naomba nikulipe, nikamuuliza wewe si umetoa pesa, umetoa bei gani? Akasema ametoa elfu 50 nikamwambia sasa mimi unaniuzia bei gani?

"Akaniambia kaka unipe elfu 20, nikamwambia haiwezekani nikatoa laki moja nikampa Mr. Nice nikamwambia kwa kuwa hii umerekodi kwa elfu hamsini chukua hii karekodi nyimbo nyingine 2, nikamwambia si ulikuwa unataka elfu 20 nikachukua elfu 20 nikampa," amesema DJ John Dillinga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live