Msanii nguli wa Bongo Fleva, Mr. Nice amesema anajisikia furaha na faraja kwa namna ambavyo anaishi na Wakenya nchini kwao kwani wamekuwa wakimkarimu kama ndugu yao.
Mr. Nice amesema hayo wakati akihojiwa na chombo kimoja cha habari nchini ambapo amesema.
"Ukiwa na pesa kila kitu kinabadilika, Nairobi kuko safi, namshukuru Mungu kama kuna majirani ambao wako bora zaidi basi ni Wakenya na hata majirani wazuri ni wale wanaokaa na boma yako.
"Wakenya wananihudumia vizuri na nipo Kenya kwa zaidi ya miaka tisa sasa, Wakenya hawajawahi kunitenda vibaya ni watu ambao wananiheshimu zaidi na kunipenda sana, nisiwe mnafiki nawapenda sana Wakenya.
"Kule Nairobi nafanya mambo mengi sana, nina Studio kule, kule wenzetu unaruhusiwa kufungua kitu chochote, kule Kenya nimefungua grocery/Pub, zinafika Pub saba, kwenye biashara hiyo niko na mke wangu ambaye ni Mkenya, nipo vizuri kiuchumi," amesema Mr. Nice.