Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mr Nice; The Multiplatinum Artist

Mr Nice 3be244 Mr Nice; The Multiplatinum Artist

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

RIAA ni CHAMA cha Tasnia ya Muziki Marekani. Wanakiita "Recording Industry Association of America". Mwaka 1958, RIAA, walitambulisha hadhi ya dhahabu (gold) ya mauzo.

Kwa mujibu wa RIAA, mwanamuziki anapouza nakala 500,000, anakuwa amefikia hadhi ya gold. Kisha, kuanzia mwaka 1976, RIAA walitambulisha “platinum” kwa mauzo yenye kufikia milioni moja.

Mauzo ya muziki yanayoanzia milioni mbili, yanaitwa “multiplatinum”, endapo yatagonga milioni 10, hiyo ni almasi (diamond).

My dear comrades, muhtasari uliotangulia ulikuwa maandalizi ya taarifa muhimu mno kwa nchi. Ni kwamba Tanzania tuna our own multiplatinum musician; ni Nice Lucas Mkenda “Mr Nice.”

Mchaga mwenye swaga za kizanzibari, alifunga magoli mengi sokoni. Nenda Mwananchi Store, ukashuhudie King’asti wa Kikulacho mwenye kuku anayepanda basikeli, alivyofanya kufuru ya mauzo.

Nakala milioni mbili za mauzo ya CD. Hiyo ni multiplatinum. Kisha kaseti (VHS), mamilioni kwa mamilioni. Legend Papa Luv Boni, ameshasimulia mara kadhaa jinsi walivyokesha wakigonga mihuri mamilioni ya VHS. Juzi usiku walikesha wanathibitisha milioni moja na nusu, leo tena, keshokutwa wanarejea mkesha. Laiti RIAA ingekuwa inafanya kazi Tanzania, leo hii Mr Nice angekuwa na tuzo yake yenye kumthibitisha kuwa multiplatinum artist. Pengine angetambulika kama diamond musician. Mr Nice was good. Very good!

Muziki wake uliingia ndani zaidi kwa watoto, akina mama wakaunga tela. Mababa hawakuwa na namna. Akauza audio na video kwa kishindo.

Hadithi ya mwamba imara. Nani hakuimba Takeu? H-Baba na “Bubu”, Mez B na “Kikuku cha Mama Rhoda”, Longomba kutoka Kenya na msako wa “Funguo”, bado Mr Nice aliendelea kutawala Takeu. Nice ni mwamba imara.

Kila saluti itapigwa. Ni Januari 26, 2024, Alliance Francaise, Upanga, Dar es Salaam. Zitafanyika sherehe za Bongo Flava Honors, kutambua mchango wa thamani kubwa wa Mr Nice, katika ujenzi na ukuaji wa Bongo Flava.

Mr Nice atatunukiwa hall of fame plaque, kisha atamvalisha bata raizoni live. Ni siku ambayo Mr Nice atapiga show ya saa mbili jukwaani kwa live band. Sugu The Jongwe ataongoza shughuli. Haitakuwa siku, bali Siku ya Mr Nice. Ndimi Luqman MALOTO

Chanzo: www.tanzaniaweb.live