Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mr. Blue atangaza ujio wake mpya

Mr Blue Bysar Mr. Blue

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki wa Hip-hop nchini Mr Blue ameweka wazi kuwa sasa ni muda wa kuletea kazi mfululizo kwa mashabiki wake huku akiwataka wachague ni ngoma gani aanze kuiachia kati ya Hip-hop, Bongofleva au Amapiano.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Blue ameweka wazi kuwa anakazi za kutosha na tofauti tofauti na yupo tayari kuzitoa hivyo mashabiki wachague aanze kutoa kigongo kipi.

Hata hivyo hajaishia hapo amewaomba mashabiki wamjibu katika upande wa ‘komenti’ kuwa ni ngoma gani ambayo wanatamani kuisikia ili aweze kuiachia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live