Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpwa wa Michael Jackson azua taharuki

Jaafar Jackson Jaafar Jackson.

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya watu Jijini Los Angeles Marekani Weekend hii walidhani wamemuona Michael Jackson kumbe alikuwa ni Jaafar Jackson akiwa amevaa kama Marehemu Michael Jackson.

Mpwa wa Michael Jackson, "Jaafar Jackson" yupo katika Muendelezo wa utayarishaji wa filamu (Biopic) ambayo itaakisi maisha ya marehemu Michael Jackson hivyo mara nyingi akiwa "Location" anaigiza baadhi ya watu hudhani wamemuona Michael Jackson, hii ni kutokana na namna ambavyo mpwa huyo amefanana sana na Marehemu.

Filamu hii maalumu kwa ajili ya kuenzi maisha ya Michael Jackson inatarajiwa kutoka Mwezi wa 4 mwaka 2025.

Mtu gani nchini Tanzania ameshafariki lakini unatamani hivi sasa itayarishwe filamu maalumu kwa ajili ya kuenzi maisha yake?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live