Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpoto: Ubunifu wa kutovaa viatu ni wa Ruge, alinionya nisimtaje

42834 Mpotopic Mpoto: Ubunifu wa kutovaa viatu ni wa Ruge, alinionya nisimtaje

Wed, 20 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Msanii wa maarufu anayefanya muziki wa kughani mashairi, Mrisho Mpoto amesema Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ndiyo sababu ya yeye kutovaa viatu.

Akihojiwa leo Jumatano Februari 20, 2019 katika kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo cha Clouds TV, Mpoto ambaye ni mkali wa kibao cha ‘Salam Zao’ amesema Ruge kwake ana mchango mkubwa katika sanaa yake mpaka hapo alipo.

Kuhusu ubunifu huo wa kutovaa viatu  alimtaka asiwe anamtaja kokote atakakohojiwa kuwa ni wazo lake.

Akielezea zaidi Mpoto amesema wakati anaanza muziki huo, Ruge alitaka awe na kitu ambacho kitamtambulisha kwa watu na kiwe tofauti.

“Tukisema rasta watu wengi wanazo, pia wazo lako la kuvaa magunia ni zuri lakini lazima uyabuni kiasi kwamba hayatakufanya watu wakuone mchafu.”

“Lakini tukija kwenye viatu, je tutakuvalisha raba au viatu gani. Hivyo mwisho wa siku katika maswali yote hayo kati yangu na Ruge ikaamuliwa niwe natembea peku na ndio maana leo mnaniona natembea bila viatu,” amesema Mpoto.

Hata hivyo Mpoto amesema huwa havai viatu pale anapohudhuria dhifa mbalimbali na kwenye sehemu hatarishi kama hospitali na chooni.

Amesema awali uimbaji wake ulikuwa haueleweki na watu wa Clouds wakati mwingine ilichukuliwa kama anaipinga Serikali, lakini Ruge alisimama na kusema ndio anautaka huohuo na kuanza kufanya naye kazi ikiwemo kuzunguka naye kwenye jukwaa la fursa ambako alikuwa mmoja wa watoa mada.

Mbali na Sanaa, Mpoto amesema pia Ruge amemsaidia katika masuala ya maisha kwani ndio sababu ya yeye kumiliki shamba la heka 50 baada ya kumkatalia kununua gari pindi alipofanyakazi na kulipwa zaidi ya Sh50 milioni na leo amekuwa msambazaji mkubwa wa matunda na mbogamboga maeneo ya jijini Dar es Salaam.



Chanzo: mwananchi.co.tz