Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpolipoli kuisimamisha Kanda ya Ziwa

Mpolipoli Pic Data Mpolipoli kuisimamisha Kanda ya Ziwa

Wed, 19 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kanda ya Ziwa mko tayariiii? Yule nyota wa muziki wa bongo fleva, Dongo Ngwegwe ‘Mpolipoli’ anatarajia kuangusha burudani kali kwa mikoa nane ya ukanda huo itakayoambatana na utamburisho wa ngoma yake mpya ya ‘Zali’.

Mkali huyo wa muziki ambaye anatesa jijini Mwanza anatarajia kufanya shoo kubwa katika Mikoa nane ya Kanda ya Ziwa, akianzia Mwanza, Mara kisha Shinyanga na ratiba nyingine kuendelea.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mpolipoli amesema baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, atafanya ‘tour’ kali kwa mikoa ya kanda ziwa akiwapa burudani wadau na mashabiki wa muziki.

Amesema lengo kubwa ya ziara hiyo ni kutanua kazi yake lakini kutengeneza njia ya kufikia malengo katika ishu ya muziki ikiwamo kupata changamoto mpya.

“Kazi itaanzia hapahapa Mwanza nikikusudia Mei 20, kisha Mara na Shinyanga na ratiba kuendelea kwa Mikoa mingine, nimejipanga kutoa burudani kwa wapenzi wa muziki” amesema Mpolimpoli.

Nyota huyo aliyewahi kutesa na nyimbo kadhaa kama ‘Umenimaliza’, ‘Kiuno dondola’ na ‘Ongeza’ amesema kibao chake kipya cha Zali anaamini kitafunika msimu huu kutokana na ujumbe uliomo ndani.

Hata hivyo, msanii huyo anayechipukia, ameongeza kuwa changamoto kubwa kwenye muziki kwa sasa ni kutegemea sana shoo kutokana na vigezo vya kufungua mitandao ya kijamii ‘Youtube’ kuwa na masharti mengi.

“Youtube kwa sasa imekuwa ngumu, masharti ni mengi na sisi wasanii tulitegemea sana huko kuliko kufanya shoo tu, ila sikati tamaa natamani siku moja kumfikia Diamond’’ amesema Msanii huyo.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz