Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpiga picha wa Diamond na begi la kilo 13

78706 Mpigapicha+pic

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kama unafuatilia mitandao ya kijamii na kuona picha na video nzuri za mwanamuziki Diamond Platnumz, nyuma ya kazi hiyo yupo Lukamba.

Huyu ni miongoni mwa wapiga picha wa mastaa waliojizolea umaarufu mkubwa kutokana na umahiri wao.

Licha ya kuwa kazi hiyo inaonekana kuwa rahisi, Lukamba anaeleza kuwa ameweza kujitofautisha na wapiga picha wengine kutokana na namna anavyoipenda kazi yake na kuifanya kwa moyo wake wote.

Hilo ndilo linalomfanya asione shida kubeba begi lenye uzito wa kilo 13 likiwa limesheheni vifaa vya kufanyia kazi zake.

Popote alipo Diamond atakuwepo Lukamba akizunguka huku na kule kupata picha nzuri, usilolijua ni kwamba kamera anayoitumia una uzito wa kilo tano.

“Kamera yangu ina kilo tano na kwenye begi kuna vitu vingine ambavyo uzito wake unafikia kilo 13, wala sioni shida kwa sababu ni kitu ninachokipenda na nafurahi kufanya kazi hii ambayo siku zote nimekuwa kuitamani  nifanye kitu kinachoonekana,” amesema.

Pia Soma

Advertisement
 

Chanzo: mwananchi.co.tz