Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpenzi wa zamani wa Niffer afunguka 'tuliachana mwaka jana'

Mpenzi Wa Zamani Wa Niffer Afunguka 'tuliachana Mwaka Jana' Mpenzi wa zamani wa Niffer afunguka 'tuliachana mwaka jana'

Wed, 16 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku chache baada ya mrembo mfanyabiashara maarufu mitandaoni Niffer kumkataa live aliyekuwa mpenzi wake kinyozi maarufu kwa jina la Shillah, jamaa huyo naye ameibuka na kueleza kwa upande wake.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Niffer alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi TV, alisema hamtambui jamaa huyo kwa kuwa hakuwa mchumba wake na hakumuoa.

Akizungumza na Wasafi TV, Shillah amesema, hataki sana kuongea kwa undani kuhusu mahusino yao lakini walidumu kwa muda mrefu lakini waliachana mwaka jana kwa kile alichosema ni 'muda tu ulifika wa kuachana'.

"Hakuna sababu yoyote labda kusema alinifumania au vipi lakini ilifika tu wakati akatamka nami nikaridhia tukaachana," alisema Shilah.

Kinyozi huyo anasema anafahamu mambo mengi kumhusu mrembo huyo sababu alianza naye mahusiano baada ya kufika mjini akiwa amekuja kusoma na kuanza kujihusisha na mambo mengine ya kujiongezea kipato lakini kwa kuwa wote wanajuana anaona ni busara kukaa kimya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live