Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpenzi amchanganyia mafaili Tiwa Savage

Tiwa Savage, Msanii Pekee Afrika Atakayetumbiza Tamasha La King Charles III.png Tiwa Savage

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, Tiwa Savage anasema alianza kupenda kuigiza kabla ya kufanya muziki lakini ‘Crush’ wake alikuwa mtu wa muziki muda wote akambadilsha mawazo.

Tiwa Savage ameshea hilo akizungumzia ujio wa Movie yake mpya ya Water & Garri itakayotoka siku ya May 10, 2024.

“Muda wote nilikuwa nataka kuigiza, ndio nilikuwa napapenda kwanza kabla ya muziki".

"Niliingia kwenye muziki sababu Crush wangu alikuwa karibu na wanamuziki nikasahau tena kuigiza nikaingia kwenye muziki” amesema Tiwa Savage

Pia amempa mashavu msanii mwenziye wa kike nchini Nigeria Simi kama ndio Malkia wa muziki wa Afrobeats.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live