Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpaka kuitwa mama si kazi rahisi – Linah

5541 26151694 1932083193775232 1249844949243920384 N E1522406098578 TZW

Sat, 31 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki Bongo, Linah amecharukia vikali wale wanaokosoa picha za watoto wa wenzao zinapowekwa mtandaoni.



Muimbaji huyo akizungumza na kipindi cha Uhondo, E Fm amesema si vizuri kwa wenye tabia hiyo kwani hadi mtu kufikia hatua ya kuitwa mama si kazi rahisi hata kidogo.

“Mimi kama mzazi ninapoona mwenzangu ameposti picha ya mtoto wake halafu anakuja mtu anasema mtoto wake mbaya, siyo vizuri kwa sababu mpaka kuitwa mama si kazi rahisi,” amesema.

“Kwa hiyo unapokuwa unamsindika mwenzako maneno ya namna hiyo inakuwa siyo vizuri, labda huyo anayeongea hivyo hajazaa, akija kuzaa hajui itakuwaje,” ameongeza.

Soma Pia; Linah hajutii kupiga picha za utupu katika ujauzito wake

Linah alijaliwa mtoto wa kwanza July 25, 2017, kwa sasa muimbaji huyo anafanya vizuri na wimbo ‘Same Boy’ ambayo amemshirikisha Rachel ikiwa ni ngoma ya pili kufanya pamoja.

Chanzo: bongo5.com