Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpaka kaburini, siwezi kusahau familia ya Diamond ilivyonitenga - Mzee Abdul

Baba Mondi Zs Mpaka kaburini, siwezi kusahau familia ya Diamond ilivyonitenga - Mzee Abdul

Tue, 6 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Abdul Juma Isack Luninze, maarufu kama Baba wa Diamond Platnumz kwa muda mrefu amekuwa akizungumziwa kuwa na matatizo chungu nzima licha ya mwanaye huyo kuogelea kwenye utajiri.

Mzee Abdul ambaye hivi karibuni alifanya mahojiano na chombo kimoja chA HABARI NCHINI Tanzania, amefunguka makubwa kuhusu safari yake ya maisha, na kubwa tangu familia yake, kwa maana ya Diamond na ndugu zake pamoja na mama yao Sandra walipomtenga mzee huyo.

Baba D amesema kwamba kwa muda mrefu amekuwa akiugua saratani ya ngozi, tatizo ambalo limemkwamisha katika mambo yake mengi ya kusaka riziki, huku akipitia changamoto lukuki katika kutafuta matibabu ya mionzi.

Mzee huyo pia aligusia kuhusu matukio ya nyuma yaliyoisambaratisha familia yake ambayo aliitaja kuwa alikuwa anaitegemea sana kabla ya ufa kuingia kati yake na Bi Sandra ambaye ni mama mzazi wa Diamond.

Licha ya kila mtu kujua kwamba mzee Abdul ndiye baba wa kumzaa Diamond, lakini mwaka jana Mama Dangote na Ricardo Momo waliibuka na kuweka wazi katika vyombo vya habari akisema kwamba Abdul siye baba halali wa Diamond kwani baba mzazi wa Diamond alikuwa anaitwa Salum Nyange na alishafariki.

Mzee Abdul alisema kwamba jambo hilo lilimuuma sana kwa kweli na kulitaja kuwa tukio moja katika maisha yake ambalo katu hawezi kulisahau kabisa mpaka anakufa na kurudi kaburini.

“Kusema kweli vitu ambavyo vilinitokea katika maisha yangu tangu niko kijana mpaka umri huu wa ukubwani vitu vingi vilitokea vibaya na vingine vizuri, ila kuna moja ambalo siwezi kulisahau.

“Kuja kutolewa katika familia ambayo nilikuwa nategemea, kusema kweli sitoweza kusahau kusema kweli kwa muda mrefu mpaka kufa kweli sitolisahau,” Mzee Abdul alieleza.

Mzee huyo ila alisisitiza kwamba yeye hana kinyongo na familia yake iliyomtenga – kwa maana ya Bi Sandra na wanawe kina Diamond na wengine.

Alisema kwamba ameshasamehe kabisa kwani hata yeye alisamehewa na wazazi wake na katu hawezi kulibeba kovu hilo moyoni hata ingawa hawezi kusahau tukio lile mpaka anakufa.

“Suala la kusamehe linakuja kwetu binadamu, vitabu vya dini vinatufunza kusamehe. Nikiwa kama mzazi ambaye ni muelewa, na mimi mwenyewe vile vile nimewahi kusamehewa hapo nyuma na wazazi wangu. Mimi kusamehe kwangu ni kitu chepesi, mimi ni mtu mwepesi wa kusamehe, nimesamehe,” Mzee Juma alisema.

Alitoa sababu ya kusamehe kwake kwa kusema kwamba siku zote kama mzazi mlezi, mtoto akikunyea kiganjani huna haja ya kikikata bali unanawa tu na kila kitu kingine kinaendelea mbele.

“Kama kuna mambo yaliyonitokea katika nafsi yangu nimesamehe kwa moyo mmoja, hata nikiingia katika ardhi ya Mwenyezi Mungu, mimi nimesamehe kabisa kama Mungu anavyosamehe. Niko na amani na sina dukuduku lolote katika moyo wangu kwa mtu yeyote aliyenikosea,” Mzee alisisitiza msamaha wake kwa familia yake iiyomtenga.

Alisema kwamba tayari ashakuwa mtu tofauti na ameanza maisha yake mapya bila familia yake licha ya kuendelea kusumbuliwa na tatizo la saratani ya Ngozi ambalo alisema linakuna na Kwenda kwa misimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live