Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moni na Country Boy (MoCo) wapewa baraka zote na Bob Junior

1873 Z1212 TZW

Thu, 25 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii na producer, Bob Junior amesema hana noma baada ya kusikia ngoma mpya ya Moni na Country Boy (MoCo) kutoa ngoma yao ‘Mwaah’ ambayo chorus yake inaelekea kufanana na ngoma yake iitwayo Nichumu Nikiss.



Muimbaji huyo amesema kilichofanywa na MoCo ni kitu kizuri kwani wameonyesha kukubali kile ambacho kimefanyika siku nyingi lakini wakakipa dhamani.

“By the way mimi naona ni wimbo fulani mzuri wa hip hop ambao wamefanya remix ya Nichumu Nikiss, ni kwamba wanaelewa nini Bongo Flava tunafanya, kwa hiyo big up kwao naona ni kitu kizuri,” amesema.

“Watu wengi waliniambia mbona ni kitu kinana na Nichumu Nikiss, so kwa upande wangu it’s ok haipaswi Watanzania kudisiana sana,” ameongeza.

Ngoma ya Nichumu Nikiss ya Bob Junior ilitoka mwaka 2012 na ngoma ya MoCo ‘Mwaah’ imetoka mwaka huu.

Chanzo: bongo5.com