Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moni Centrozone afunguka kutaka kujiua kisa penzi la Nai

Moni Nai Moni Centrozone na Nai

Thu, 29 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moni Centrozone; ni msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania ambaye amefunguka kuhusu madai kuwa alitaka kujiua kutokana na mapenzi baada ya kuachana na mpenzi wake, video vixen Nai mwanzoni mwa mwaka 2020.

Moni anasema kuwa, hilo halikumsumbua kutokana na namna akili yake aliyokuwa ameiweka ndiyo sababu hata mwishoni mwa mwaka 2020 aliachia ngoma kali kama Maelekezo Chapter One.

“Stori ya kutaka kunywa sumu ilikuwa ni uvumi tu," anasema Moni ambaye sasa anatamba na Ngoma ya Read Again akimshirikisha G Nako.

Moni anakiri kuwa, kuachana na mapenzi, kwa wakati huo kuna mambo mengi kwake yalikuwa hayapo sawa kutokana na janga la Corona lililosababisha shoo kutokuwepo kabisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live