Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mondi amewatega mashabiki wake

DIAMOND Mondi amewatega mashabiki wake

Mon, 5 Jul 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

NAMBA zinaonyesha Diamond Platnumz ndiye msanii mwenye mashabiki wengi zaidi nchini. Instagram ana wafuasi zaidi ya milioni 12, sawa na asilimia 20 ya Watanzania wote, wakati Youtube ana wafuasi milioni 25, hiyo ni sawa na nusu ya Tanzania nzima.

Hata hivyo, licha ya Mondi kuwaunganisha watu wote hao, kuna nyakati staa huyo wa mdundo mkali wa Kamata huwapitisha mashabiki wake kwenye njiapanda ya kuchagua kuendelea kuwa karibu yake au kujitenga naye. Ni nyakati zipi hizo.

SIMBA DAY

Mwaka 2020 Diamond alipewa dili la kunogesha sikukuu ya Klabu ya Wekundu wa Msimbazi, Simba, maarufu Simba Day iliyofanyika viwanja vya Mkapa, Dar es Salaam. Dili ambalo lilimlazimu Mondi kutengeneza wimbo maalumu wa kuisifia Simba na kupiga shoo.

Diamond alipiga bonge moja la shoo. Picha linaanza Diamond aliingia uwanjani hapo kwa helkopta na aliposhuka, chini kulikuwa na wacheza shoo zaidi ya 50 wakimsubiri kuambatana naye katika kutoa burudani.

Lakini shoo hiyo iliwakera mashabiki wa Yanga ambao pia walikuwa wanamkubali Diamond, na walionyesha hasira zao wazi kwa kuandika maoni karibu kwenye kila post aliyokuwa akiweka staa huyo kwenye mitandao yake ya kijamii.

Kwa sababu hiyo, Mondi ilibidi atoke hadharani na kutolea ufafanuzi kila kilichotokea; aliandika “Mashabiki wangu wapendwa Yanga msiumie, mimi bado ni wenu na jukumu langu ni kuburudisha.”

SIASA

Diamond amewahi kubainisha lina-pokuja suala la siasa yeye ni mpenzi wa sera za Chama cha Mapinduzi, CCM. Hata hivyo, ni wazi kwenye mashabiki lukuki aliokuwa nao kutakuwa na wengine wenye mapenzi na vyama vya upinzani kama kama vile CUF, Chadema na ACT Wazalendo.

Kwenye uchaguzi mkuu uliopita Diamond alionekana kuwa karibu zaidi na CCM, alifanya shoo kwenye mikutano yote mikubwa ya kampeni za CCM, pia alifanya intavyuu kupitia redio yake ya Wasafi akielezea jinsi sera za CCM zilivyowasaidia watanzania, kwa mtazamo wake.

Hata hivyo, mashabiki wa Diamond ambao pia ni wapenzi wa vyama vya upinzani walionekana kuchikizwa na hali hiyo kiasi kwamba walianza kumshambulia kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo lililosababisha Diamond atolee ufafanuzi kupitia mahojiano na chombo kimoja cha habari nchini yaliyofanyika kwenye mkutano wa kampeni za CCM mkoani Mwanza.

Diamond alifunguka kuwa yeye haendi kutumbuiza kwenye shoo za CCM kama msanii anayelipwa kutumbuiza, bali anakwenda kwa sababu ni mwanachama wa CCM anayetaka kukisaidia chama chake kushinda.

“Ni haki yangu kuwa mwanachama wa chama chochote ninachokipenda, kwahiyo wapinzani wa CCM waendelee kuwa upinzani lakini wasinizuie na mimi kuendelea kubaki CCM,” anaema Diamond.

ZARI

Mapenzi ni sehemu ya ustaa wa Diamond tangu alipoanza kutoka na mrembo Wema Sepetu zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Walipomwagana na Wema, Diamond akawa na warembo wengine kabla ya mwaka 2014 kuangukia mikononi mwa mganda, Zari The Bossy Lady ambaye amezaa naye watoto wawili.

Kwa sasa wawili hao sio wapenzi tena, lakini inaonekana Diamond yupo karibu zaidi na Zari kuliko mwanamke yeyote kati ya aliowahi kuwa nao. Lakini kwa bahati mbaya, pia Zari amekuwa kwenye mabifu karibu na wanawake wote waliowahi kuwa na Diamond. Zari amewahi kuwa na vita na Wema Sepetu na inaendelea mara kwa mara huko Instagram, amewahi kuwa na vita na Hamisa, pia kupigana vijembe na Tanasha.

Sasa ubaya ni kwamba, mashabiki wa Diamond hasa wa kike pia wanatamani kumpangia msanii wao mwanamke wa kuwa naye kiasi kwamba, wasiompenda Zari hujikuta njia panda Diamond ya kuendelea kumshabikia Mondi kila anapoonyesha kuwa karibu na Zari.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz