Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mondi Akiri Kuchezea Wanawake

DIAMOND 3 Mondi Akiri Kuchezea Wanawake

Sun, 27 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SUPASTAA wa muziki nchini Tanzania, Nasibu Abdul almaafuru Diamond Platnumz amesikika akijipiga kifua na kukiri kuwa ana uwezo mkubwa wa kuvutia wanawake wengi na kuwachezea (kuwa kiwembe).

Kupitia kampuni ya filamu ya Netflix katika maandalizi yake ya kuzindua documentary (kipindi cha runingani cha maisha ya alipotoka hadi alipofikia kwenye mafanikio) yenye jina la Young, Famous and African itakayozinduliwa Machi 18, mwaka huu, huko ndiko Diamond au Mondi anakosikika akikiri hilo wakati akijibizana na mama wa watoto wake wawili, Zarinah Hassan almaarufu Zari The Boss Lady.

ATAZAMWA NCHI 190

Shoo hiyo ambayo inasubiriwa kwa shauku itaangazia maisha ya baadhi ya watu maarufu na tajiri barani Afrika wakiwemo Diamond kutoka Tanzania na mfanyibiashara Zari kutoka Uganda, mwenye maskani yake, Durban nchini Africa Kusini. Wengine ni Nadia Nakai na mtangazaji Andile Ncube kutoka Afrika Kusini, waimbaji Annie Macaulay-Idibia na 2Baba kutoka Nigeria.

Shoo hiyo imetayarishwa na Peace Hyde; raia wa Ghana na mwakilishi wa Netflix barani Afrika ambaye amejishindia tuzo kadhaa kutokana na kazi yake. Ikumbukwe kuwa, Netflix yenye makao yake makuu California nchini Marekani ni huduma namba moja duniani ya kutazama video za muziki, filamu na tamthiliya kwa njia ya kuzitazama kupitia huduma ya intaneti, kimombo ‘streaming’.

Shoo hiyo itaruka kwenye jukwaa la Netflix mtandaoni na kutazamwa na nchi zipatazo 190, ambazo kwa jumla zina watumiaji wa Netflix milioni laki mbili na zaidi.

DIAMOND ATAMBA

Katika video fupi ya utambulisho wa shoo hiyo ambayo Zari ameiachia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, inaonesha mastaa waliohusika katika kipindi hicho wanafichua mengi kuhusu maisha yao.

Katika video hiyo, Diamond anasikika akitamba kuwa ana uwezo mkubwa wa kuvutia wanawake wengi na kuwachezea. “Ninajijua, mimi ni player (mwanaume anayechezea wanawake kimapenzi),” anasikika Mondi akikiri huku akionekana kujivunia jambo hilo.

ZARI: ULIHARIBU

Kwa upande wake, Zari ambaye ni eksi na mama wa watoto wake wawili, naye anasikika akimwambia Mondi kwamba jambo hilo ndilo lililotia doa kwenye penzi. “Uliharibu,” anasikika Zari akimwambia Diamond katika video hiyo.

Katika shoo hiyo ya Young, Famous and African, Diamond pia anakiri kwamba kuwa mtu maarufu, tajiri na mwenye umri mdogo ni jambo nzuri mno maishani.

WANAWAKE WA DIAMOND

Diamond ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na ubabe wake katika muziki barani Africa anafahamika kuwa aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na zaidi ya wanawake kumi kutoka mataifa mbalimbali.

Miongoni wao ni Wema Sepetu, Hamisa Mobeto, Irene Lous au Lyyn, Zari, Tanasha Donna na wengineo huku madai ya kutoka na msanii wake, Zuhura Othman almaarufu Zuchu yakiendelea mitandaoni. Hivi karibuni Diamond alikiri kuwa kwenye uhusiano mwingine kwa sasa ila hakufichua jina la mchumba wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live