Mwigizaji Yvonne Cherrie "Monalisa" ameacha swali kupitia ukurasa wake wa instagram kuwa anahitaji apewe maua yake akiwa hai ya kuibeba tasnia ya Filamu Tanzania.
Mwigizaji Yvonne Cherrie "Monalisa" ameacha swali kupitia ukurasa wake wa instagram kuwa anahitaji apewe maua yake akiwa hai ya kuibeba tasnia ya Filamu Tanzania. “LIFE TIME ACHIEVEMENT AWARD, Kuna siku nitaipata hii TUZO nikiwa hai au nikiwa nimekufa. Watasema, “Alikuwa mmoja wa wasanii wa kwanza katika Kiwanda cha Filamu Tz, alishawishi wasanii wengi kuingia katika Filamu, alikuwa NEMBO ya Filamu Tanzania. Niambieni basi nikiwa hai, NASTAHILI.”