Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mohbad alikuwa hai akiwa Hospitali - Shabiki

Dfh Ohbad Mohbad alikuwa hai akiwa Hospitali - Shabiki

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Kituo cha Afya cha Perez Medcare kukanusha kumpokea Msanii Marehemu wa Nigeria Mohbad akiwa hai katika Hospitali yao, na pia kusema Nesi aliyemchoma sindano Mohbad sio mfanyakazi wao.

Mapya mengine yameibuka kuhusu kifo cha Mohbad baada ya kuwepo kwa Voice inayosambaa Mitandaoni, Ambapo Shuhuda anadai alishihudia Mohbad akiwa hai amezidiwa siku aliyopelekwa hispitali.

Shuhuda huyo amedai Mohbad alipelekwa Hospitali na Rafiki yake ambaye alionekana kwenye ile Video akipiga kelele kwamba Mohbad amefariki Dunia. Hivyo maswali mengi ambayo yapo vichwani mwawatu kuhusu Kifo cha Mohbad yeye ndiye atakuwa na Majibu ya kutosha.

"Nilifanikiwa kumuona Mohbad Hospitali nilishtuka na kuwaomba ma Nesi kupiga nae picha na kumueleza kuwa nimekuwa nikisikiliza sana nyimbo zake, ila kuna Nesi mmoja alininong'oneza kuwa wamemchoma sindano.

Ndipo yule Jamaa aliyemleta Mohbad Hospitali ghafla akatoka na mwili wa Mohbad Hospitali akiwa kifua wazi . "Sasa ni kawa najiuliza mbona haraka haraka sana hivi inakuaje na huyu mtu ni mgonjwa?"

Ikumbukwe kwamba Mohbad alifariki dunia Septemba 12 mwaka huu na kuzikwa masaa machache tokea kifo chake kitokee huko Nigeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live