Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mobetto na Rayvanny wahojiwa, waachiwa

62916 Pic+rayvan Mobetto na Rayvanny wahojiwa, waachiwa

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Mwandishi WetuMore by this Author Dar es Salaam. Video ya msanii Shaban Mwakyusa maarufu Rayvanny na Paula mitandaoni yaibua mapya. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mkali huyo wa wimbo wa Kiuno na Teamo  na mwanamitindo Hamisa Mobetto kuhojiwa polisi kwa zaidi ya saa mbili  na kisha kuachiwa.

Walifika kituo cha polisi Oysterbay jana Jumanne Februari 16, 2021 na kuhojiwa kwa zaidi ya saa mbii kuhusu tuhuma za Kajala kwamba Mobetto ndio alimpeleka binti yake kwa Rayvanny, baada ya kumuomba atoke naye kwa ajili ya chakula cha mchana



Rayvanny

Shutuma hizo zilijibiwa na Hamisa kupitia mtandao wa Instagram ,  ambaye mbali na kukanusha kupitia mwanasheria wake alimuandikia barua Kajala kumtaka akanushe alichokisema ndani ya saa 12 kabla hajamfungulia mashtaka ya kumchafulia jina. Akizungumza na Mwananchi Digital Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai amesema wasanii hao walijisalimisha kituo cha Polisi Kawe, kabla ya kuhamishiwa Oysterbay kwa mahojiano zaidi.



“Hivi ninavyokupigia simu wanamalizia taratibu waondoke, maana wameshamaliza mahojiano, ”amesema Kingai jana saa 4:12 usiku.
Chanzo: mwanaspoti.co.tz