Mjasiriamali Hamisa Mobetto amefichua kwamba hana mchoro wowote wa tattoo katika mwili wake wala hajawahi fanyiwa upasuaji wa aina yoyote katika uso wake.
Mobetto ambaye alikuwa live kupitia Instagram alasiri ya Jumanne aliweka wazi kwamba alikuwa radhi kujibu kila aina ya maswali kutoka kwa mashabiki wake.
Katika kipindi hicho kilichodumu kwa Zaidi ya nusu saa hivi, wengi waliweza kumtupia maswali mengi na magumu lakini mrembo huyo mama wa watoto wawili aliweza kuyajibu kadri ya uwezo wake.
Mmoja alimuuliza iwapo ana tattoo au kufanya sajari jambo ambalo alikanusha, jambo kwa sajari, alisema tu kwamba uso wake haujawahi fanyiwa uppasuaji wowote lakini hakuweza kubainisha hali vipi kuhusu sehemu zingine za mwili wake wenye ulimbwende uliopitiliza.
“Mimi sina tattoo hata moja kwenye mwili wangu, sipendi tu lakini napenda kuziona kwenye miili za watu lakini sio kwangu. Pia mimi sijawahi fanya upasuaji wowote kwenye uso wangu. Si mnaona uso wangu ulivyo kama nilivyozaliwa, hakuna uboreshaji wa sajari,” Mobetto alisema huku akisogeza uso wake karibu na kamera huku pia akisogeza nywele kwenda nyuma ya kichwa.
Mama wa watoto wawili aliweza kuzungumzia pia kuhusu mipango ya kuongeza watoto wengine na mwanamume wake Kevin kutoka Togo.
“Ndio nina mpango wa kuwa na watoto wengi. Kama mwenyezi Mungu atanijaalia nataka niwe na watoto angalau watano au saba hivi lakini sio kwa sasa hivi, pengine baada ya miaka kama mitatu kuanzia sasa hivi,” alifichua.