Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mobetto: Nimekutana na wanaume wengi, ila huyu wa sasa ni kiboko

Mobetto Na Mpenzi Wake Mahaba Mobetto: Nimekutana na wanaume wengi, ila huyu wa sasa ni kiboko

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamitindo maarafu wa Bongo, Hamisa Mobetto amemwagia sifa mpenzi wake wa sasa, Kevin Sowax ambaye ni mfanyabiashara maarufu Afrika na CEO wa Kampuni za Twinsk Company na Lemimozart Restaurant.

Raia wa Togo, Kevin Sowax ndiye ameushikilia moyo wa Hamisa kwa wakati huu, wawili hao wamekuwa pamoja Tanzania kwa zaidi ya wiki moja hivi wakifurahia harufu nzuri ya karafuu visiwani Zanzibar mwezi uliopita.

"Huyu wa sasa ana moyo mzuri sana, ana moyo wa kitofauti sana, nimekutana na wengi lakini yeye yupo tofauti kwa kila kitu, yaani katika mahusiano yangu yote yaliyopita sina wa kumfananisha nae.

"Nimekuwa kwenye mahusiano na wanaume tofauti-tofauti na wote huwa wana tabia moja, lakini huyu yuko tofauti kabisa ananipa mapenzi ya kitofauti ambayo sijawahi kuyapata popote," amesema Hamissa Mobetto.

Katika historia yake, Hamisa ambaye ni mama wa watoto wawili sio mtu wa kuweka sana hadharani mahusiano yake, ni vigumu kupata picha nyingi zake akiwa na wazazi wenziye, Majizzo na Diamond, hii ni kutokana na usiri au mtindo wake wa maisha kipindi yupo nao.

Lakini sasa mambo yamebadilika na yanaenda mbio, Hamisa ameweka wazi kila kitu kuhusu Kevin na hata kumtambulisha kwa mama yake mzazi, ni Hamisa ambaye hakuzoeleka kwa miaka zaidi ya 10 ya umaarufu wake katika kiwanda cha mitindo, filamu na muziki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live