Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mobetto: Diamond kutomposti Dylan hainiongezei chochote

Mobeto Diamond Mama D Mobetto: Diamond kutomposti Dylan hainiongezei chochote

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kupitia Amplifaya ya Clouds Fm, mrembo na mwanamitindo Hamisa Mobetto amejibu sababu za kwanini mzazi mwenzie, Diamond Platnumz hakum-post mtoto wao, Dylan kivyovyote vile siku ya birthday yake August 08 mwaka huu.

Hamisa amedai hajui sababu ni nini, uwenda hilo swali angeulizwa Diamond mwenyewe. Hamisa pia ameeleza kuwa Baba yake hakuwahi kuwa na Instagram, hivyo Hamisa hakuwahi postiwa na haikuongeza wala kupunguza kitu mbali na ilivyotakiwa.

Kuhusu kama bado Msanii huyo (Diamond) anaendelea kutoa matunzo kwa mtoto wake, Hamisa hakutaka kuweka wazi ishu hiyo.

Ikumbukwe tu baada ya Diamond kutoshare kwa namna yoyote ile birthday ya mtoto wake August 08 mwaka huu, Mama mzazi wa Dylan, Hamisa Mobetto alimfuta Diamond kwenye Bio ya Instagram page ya Dylan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live