Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mobeto kumburuza Diamond kortini tena!

Mobeto Diamond Mama D Mobeto kumburuza Diamond kortini tena!

Mon, 29 Aug 2022 Chanzo: Global Publishers

Hamisa Hassan Mobeto; ni mwanamama maarufu nchini Tanzania akidaiwa kuwapiku warembo wote mjini ambaye sasa amechafukwa na kutonesha kidonda cha mzazi mwenzake ambaye ni staa mkubwa wa muziki, Nasibu Abdul almaarufu Diamond Platnumz, IJUMAA lina mkanda kamili.

KORTINI TENA

Watu wa karibu wa Mobeto wanadai kuwa, mrembo huyo ametangaza vita upya na ex wake huyo huku akieleza waziwazi kusudio la kumburuza kortini kwa mara nyingine.

Februari, 2018, Mobeto alimburuza mahakamani Diamond au Mondi akidai matunzo ya mtoto wao wa kiume aitwaye Dyllan.

Katika shauri hilo lililofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar, wawili hao walisuluhishwa na kukubaliana kuhusu matunzo ya mtoto wao huyo.

Baada ya suluhisho hilo, Mobeto aliliambia gazeti hili la IJUMAA kuwa; “Maamuzi nimeridhika nayo na tumekubaliana kuhusu matunzo ya mtoto. Pande zote mbili tulikaa na kukubaliana, nashukuru kila mtu tumekubaliana na nimeridhika…”

Kwa upande wake Diamond alisema; “Tutaangalia jinsi ya kumtunza mtoto wetu, tunategemea baadaye anaweza kuwa kiongozi f’lani, nawashauri wazazi wa kike na kiume kuweka majivuno pembeni kwani mwisho wa siku anayeathirika ni mtoto.”

VITA UPYA

Pamoja na makubaliano hayo ambapo Diamond alikubali kumtunza mtoto wao huyo, lakini upande wa Mobeto umeanzisha vita upya huku ukishusha madai mazito kuwa, jamaa huyo hatoi matunzo ya mtoto.

Akizungumzia madai hayo, Mobeto amefunguka mazito akionekana kabisa kuwa na jambo zito moyoni akisema; “Sina muda wa kumbembeleza baba mtoto wangu (Diamond), yeye ni mtu mzima na anajua kama ni mtoto wake, sielewi kwa nini anambagua.”

MAJIBU YA DNA

Hata hivyo, juu ya sakata hilo la mtoto wa Mobeto na Diamond kumekuwa na madai ya muda mrefu kwamba, huwenda familia ya jamaa huyo haiamini kama mtoto huyo ni damu yao.

Lakini katika majibu aliyoyatoa Mobeto Oktoba, 2020, ni kweli yeye na Diamond walifanya vipimo vya DNA ili kujihakikishia na majibu yalitoka asilimia 100% mtoto huyo ni wa Diamond.

Mobeto alisema; “Tulikwenda hospitalini na tukachukuliwa vipimo vinnevinne, wakasema tusubirie wiki mbili au tatu na majibu yakatoka mtoto kwa asilimia zote 100% ni wa Diamond.”

MAMA DANGOTE ATAJWA

Hata hivyo, juu ya sakata hilo, mama mzazi wa Diamond, Mama Dangote amekuwa akitajwa na kutupiwa lawama kuwa ndiye chanzo cha mtoto wa Mobeto kutelekezwa kwa sababu za ugomvi wao binafsi.

Baadhi ya watu wameendelea kumtetea mtoto huyo kuwa hana makosa hivyo kuendelea kufanya hivyo ni kumuumiza malaika wa Mungu asiyejua lolote.

Wanasema kuwa, ifike mahali Mama Dangote aachane na bifu na Hamisa amkutanishe mtoto huyo na watoto wengine wa Diamond la sivyo dhambi hiyo itamtafuna.

Watu hao wanaohoji ni kosa gani mjukuu wake huyo alimtendea ambalo halisameheki?Wanamtaka Diamond kuonesha msimamo kwa watoto wake kwa sababu wakati akiwatafuta alikuwa yeye na mwanamke husika.

Mbali na Dyllan aliyezaa na Mobeto, Dimond ana watoto wengine watatu; wawili amezaa na mwanamama maarufu Afrika Mashariki akitokea Uganda, Zari The Boss Lady na mwingine amezaa na mwanamama Tanasha Donna ambaye ni msanii wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Kenya.

Chanzo: Global Publishers