Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mobeto hana mpango wa kuzaa kwa sasa

Mobetto.jpeg Mobeto hana mpango wa kuzaa kwa sasa

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamitindo na staa wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto amesema kwa sasa hana mpango wa kuzaa kwani tayari anao watoto wawili wa kike na wa kiume.

Mobeto ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akifanya mahojiano na waandishi wa habari ambapo alisema hata hivyo mpenzi wake wa sasa, hajamuomba kuzaa naye.

“Nashukuru mkaka wa watu hata hajaniambia anataka mtoto lakini pia kwa sasa sihitaji kuzaa labda huko baadaye nitakapoingia kwenye ndoa Mungu akipenda maana tayari ninao watoto wawili wa kike na wa kiume,” alisema Mobeto.

Mobeto alisema mwanaume wake wa sasa ambaye amemzawadia Range Rover hivi karibuni, hahitaji kumuanika mitandaoni kama ilivyokuwa kwa wengine kwani hataki yatokee yale ya kuachika na kuwa mtu wa kutambulisha mwanaume mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live