Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mobeto amfikia Wema

Wema Na Mobeto Mobeto amfikia Wema

Tue, 16 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hamisa Mobeto; ni mwanamitindo, muigizaji na mwimbaji maarufu nchini Tanzania ambaye hatimaye amemfikia malkia wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu kwa kuwa na idadi sawa ya wafuasi kwenye Mtandao wa Instagram; wote kwa sasa wana zaidi ya wafuasi milioni 9.8.

Wengi wanajiuliza ni nini kimesababisha umaarufu wa Wema kushuka huku ule wa Hamisa ukipaa kila kukicha.

Wapo wanaosema Hamisa amebebwa na kujiingiza kwenye muziki, kuzaa na ma-C.E.O wawili, Majizo na Diamond Platnumz kisha ukaribu wake na rapa Rock Ross wa Marekani hivyo kumfanya kuwa midomoni mwa mashabiki wake kila kukicha.

Wengi wanasema kuwa, Hamisa amejua kucheza na akili za wafuasi wake kwa kujua wanataka nini na kuwapa hasa stori za udaku ambazo wengi wanazipenda kutoka kwake.

Kwa upande wake Wema wanasema ameshindwa kucheza na hisia za mashabiki wake kama zamani na kuwamba udaku hasa baada ya kuamua kumficha mwanaume wake wa sasa kisha kuhusishwa kudeti na watu kama PCK na Whozu ambayo eti wamemshusha dizaini f’lani kwani alitakiwa kuwa na staa mkubwa kama ilivyokuwa enzi zake na Diamond.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live