Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mobeto afunguka ugomvi wake na Wema

Wema Na Mobetoo Mobeto afunguka ugomvi wake na Wema

Mon, 14 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo anayefanya poa kunako anga la burudani Bongo, Hamisa Mobeto amefunguka ishu ya kuwa bifu na muigizaji Wema Sepetu ambalo chimbuko lake ni kufikisha followers Mil 10 kwenye mtandao wa Instagram.

Amesema licha ya Wema kusema hataki kushindanishwa kufautia ishu hiyo lakini yeye pia hana tatizo naye kwani anachokiangalia yeye, wafuasi hao wanampa madili ya matangazo basi!

"Mimi sina tatizo na Wema. Mimi ninachoangalia ni followers wangu ambao kwangu ni biashara kama unavyoona nawatumia sana katika matangazo. Mimi hata nisipopost kwa wiki nzima bado utaona followers wanaongezeka tu.

"Tena mimi nisipoposti mashabiki zangu ambao ndio wananijua vizuri huwa wananiuliza kwa nini siposti na kuniomba niposti," alitamba Mobeto.

Vita ya followers kwa Mobeto na Wema ilikolezwa zaidi na mashabiki ambao walimsema Wema kuwa anazidiwa na Mobeto jambo ambalo lilimkera Wema na kusema hataki kushindanishwa.

Kwa sasa, Wema ana wafuasi Mil. 10.1 huku Mobeto akiwa na Mil. 10.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live