Mwanamitindo na Mjasiriamali, Hamissa Mobeto amefunguka kuwa alishawahi kutolewa posa mara nyingi na posa ndogo ilikuwa ni milioni 10.
"Nilishawahi kutolewa posa mara nyingi sana na wengine siwafahamu na wengine nawafahamu lakini unakuta mambo hayajakaa sawa maana suala la ndoa ni la kujipanga.
"Posa ndogo ambayo ilishawahi kuja nyumbani ilikuwa million kumi. Mimi nina watoto na nimekuwa kwenye mazingira ya kushuhudia baadhi ya ndugu zangu wananyanyasika sababu hawana na chao hivyo kabla sijaingia kwenye ndoa nataka nijikamilishe ili hata nikiingia niwe full na hata miaka ya mbele ikishindikana basi niwe na vyangu," amesema Mobeto.
Kumbuka Mobeto ni mama wa watoto wawili, mmoja amezaa na mkurugenzi wa Efm na ETV, Majizzo na Mwingine amezaa na msanii wa Kimataifa, Diamond Platnumz.