Mrembo anayefanya poa kwenye gemu la Bongo Fleva, Hamisa Mobeto, ameweka wazi kuwa kwenye mishe zake za muziki, amefanya kazi na mmoja wa wanamuziki wanaounda bendi ya Sauti Sol kutoka nchini Kenya.
Akipiga stori mbili tatu na media wikiendi iliyopita, Mobeto alisanua jambo hilo kwa kusema, anayo ngoma hiyo kwenye kabati lake lakini anasikilizia menejimenti yake waseme ni lini wataliachia.
"Nilifanya na mmoja wa memba wa Sauti Sol ipo tu ndani tangu mwaka jana so muda wowote itaachiwa," alisema Mobeto.
Alipoulizwa kama msanii huyo ambaye amefanya naye kama hajamuuliza kuhusu kuiachia, akasema ni kweli mwamba ameiulizia lakini yeye ameliacha kwa uongozi wake.