Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mobeto, Uwoya waomba radhi kwa kuanika picha zao za utupu

11786 Uwoya+pic.png TanzaniaWeb

Thu, 19 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wasanii Hamisa Mobeto na Irene Uwoya wameomba radhi kwa kosa la kuweka picha za utupu katika mitandao ya kijamii.

Wamechukua uamuzi huo saa chache baada ya kutakiwa kufanya hivyo na kamati ya maudhui ya mamlaka ya mawasiliano (TCRA).

Uamuzi wa TCRA umetolewa leo asubuhi Alhamisi Julai 19, 2018 baada ya wasanii hao kukiri kosa katika mkutano uliowahusisha waandishi wa habari.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Valeri Msoka amesema Hamisa alifanya kosa la kuweka mtandaoni picha za ujauzito na Irene kuweka picha zake za nusu utupu, akiwa ufukweni.

Kupitia kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Instagram, Uwoya ndio alikuwa wa kwanza kuomba radhi kwa kuweka picha anayoonekana amejilaza huku sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa wazi.

“Wapenzi wangu, ndugu zangu, wakubwa zangu na wadogo zangu naomba radhi kwa picha niliyopost ...,najua nimekwaza, sikujua nitawakwaza sababu ya role mode wangu Beyonce, nimejifunza sasa …,nawapenda,"

Kwa upande wake Mobeto ameandika, “husika na kichwa cha habari hapo juu, mimi ni Hamisa Mobeto ambaye ni mfanyabiashara wa mitindo, naomba kutumia  fursa hii kuomba radhi kwa watanzania na wengine wote ambao ni watumiaji wa mitandao. Ni kuhusiana na kitendo cha mimi na mashabiki zangu kutuma picha zangu zinazoonyesha nusu utupu kwenye page zao za Instagram.”

Amesema, “Pia natumia fursa hii kuwashukuru kamati ya maudhui kwa jinsi walivyoniita kwenye kamati yao na kunipa nafasi ya kujitetea na mwisho kufanya uamuzi wenye haki kwangu na kwa wapenzi wangu wote.”

VIDEO: Uwoya na Mobeto kikaangoni, watakiwa kuomba radhi

 

Chanzo: mwananchi.co.tz