Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mobeto: Sitaki wanaume Watanzania

Mobetto.jpeg Mobeto: Sitaki wanaume Watanzania

Thu, 29 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hamisa Hassan Mobeto; ni mwanamitindo, muigizaji na muimbaji wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambaye amefunguka kuchukizwa na tabia za wanaume wa Kitanzania.

Hamisa anasema kuwa, anachukizwa na tabia zao za kuwatumia wanawake na kuwatelekeza baada ya kumaliza shida zao.

“Sitaki wanaume wa hapa Tanzania kwa sasa,” anasema Hamisa ambaye ni mama wa watoto wawili; mmoja amezaa na Majizzo na mwingine amezaa na Diamond Platnumz.

Tetesi ni kwamba kwa sasa Hamisa ni ‘chakula’ ya mheshimiwa mmoja hapa Tanzania (ni Mtanzania) ambaye hivi karibuni alimzawadia gario la kifahari aina ya Range Rover Evoque.

Hayo yanakuja miezi kadhaa baada ya Hamisa kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Rapa wa Marekani, Rick Ross au Madevu.

Kumbukumbu zinaonesha kwamba, Hamisa amepata kuhangaika na midume ya Kibongo hivyo kuna uwezekano akawa amejifunza mengi kutoka kwao ndiyo maana amefikia hitimisho hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live