Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mobeto: Mambo ya Chumbani Siwezi Kunaniliu....

Mobetoz Mobeto

Sun, 13 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWANAMITINDO wa kimataifa na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto anafunguka kuwa, kamwe hawezi kumshauri mtu yeyote juu ya uhusiano wake wa kimapenzi (mambo ya chumbani) kwa sababu hata yeye alishauriwa na wengi, lakini haikwenda hivyo.

Hamisa anasema kuwa, katika mambo ya uhusiano wa kimapenzi ni vigumu kumshauri mtu hata siku moja kwa sababu hata yeye alipokuwa kwenye mapenzi walijitokeza watu mbalimbali na kumshauri, lakini hakuwaelewa, badala yake akaendelea na mambo yake.

“Kwenye mapenzi siwezi kumshauri mtu yeyote hata rafiki yangu wa damu maana ni jambo ambalo ni gumu kumwambia mtu akakuelewa kwa sababu hata mimi walijaribu kunishauri nilipokuwa kwenye uhusiano wangu na ilishindikana mpaka mwenyewe nilipoamua kufanya uamuzi wangu,” anasema Hamisa ambaye aliwahi kuwa kwenye uhusiano na kuzaa na DJ Majizo na Diamond Platnumz.q

Chanzo: www.tanzaniaweb.live