Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mnigeria avunja rekodi ya Dunia

Tunde Onakoya (5).jpeg Tunde Onakoya.

Sun, 21 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bingwa wa chess Nigeria na mtetezi wa elimu ya watoto amefanikiwa kucheza chess bila kusimama kwa saa 60 katika eneo la Times Square mjini New York City akivunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kucheza muda mrefu zaidi.

Tunde Onakoya, 29, anatarajia kukusanya dola milioni 1 kwa ajili ya kusaidia elimu ya watoto kote barani Afrika kupitia jaribio lake la kuweka rekodi ya Dunia aliloanza Jumatano.

Alikuwa amepanga kucheza mchezo huo kwa saa 58 lakini aliendelea hadi akafikisha saa 60 saa 6:40 usiku wa Jumamosi, na kupita rekodi ya sasa ya mbio za chess ya saa 56, dakika 9 na sekunde 37, iliyowekwa mwaka 2018 na wanorway - Hallvard Haug Flatebø na Sjur Ferkingstad.

Shirika la Rekodi ya Dunia ya Guinness bado halijatoa maoni kuhusu jaribio la Onakoya. Wakati mwingine huchukua wiki kwa shirika kuthibitisha rekodi yoyote mpya. Onakoya alicheza dhidi ya Shawn Martinez, bingwa wa chess wa Marekani, kulingana na miongozo ya Rekodi ya Dunia ya Guinness kwamba jaribio lolote la kuvunja rekodi hiyo lazima lifanywe na wachezaji wawili ambao wangecheza mfululizo kwa muda wote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live